WhatsApp mara kwa mara imekua ikileta vipengele vipya au kuboresha vile ambavyo tayari vipo kwa kuvifanyia masasisho (Updates).
Kwa sasa WhatsApp wanakuja na kipengele kipya ambacho kinajikita zaidi katika swala zima la ulinzi na usalama ndani ya App hiyo hususani katika eneo la kupigiwa simu.
Labda niulize swali? Kwani wewe ukipigiwa kwa namba mpya huwa unapokea? Kama unapokea jua wengi pia wako tofauti na wewe.
Unaweza kujiuliza ni kwa nini mtandao wa WhatsApp umeamua kufikia maamuzi ya kuzuia viashiria vyote kwamba unapigiwa na namba mpya (ambayo haipo katika kitabu chako cha namba)?
Jibu ni rahisi kabisa, wamefanya hivyo makusudi ili kukulinda wewe na spams, wezi wa mtandaoni na hata kupuguza ile ghadhabu ya kupigiwa na watu wengi ambao huwajui.
Ili kuwezesha kipengele hiki unaenda katika eneo la settings >> Privacy na kisha washa eneo la Silence Unknown Callers.
Ukiwasha kipengele hiki jua hupata notification yeyote ya sauti au hata maandishi kwamba kuna simu inaingia lakini ukiingia katika mtandao wa WhatsApp na kisha kwenda katika eneo la Calls basi utaweza kuona namba hizo (zilizokua zinakupigia) huku pembeni kukiwa na kiashiria kuwa namba hizo ni mpya.
Mitandao mingi ya kijamii huwa inatumia nguvu nyingi na ya ziada katika kuhakikisha kwamba inalinda ulinzi na usalama wa watumiaji wake kwa gharama yeyote
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unadhani ni sawa kwa kampuni kufanya hivi au ndi bora wangeacha kama zamani tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.