WhatsApp wameonekana kutimiza kile walichokuwa wamekisima kwa kusitisha kabisa huduma ya WhatsApp kwa baadhi ya simu janja kuanzia Desemba 31 2017.
Simu ambazo zimekumbwa na mkasa wa kukosa kabisa huduma ya WhatsApp ni BlackBerry OS na Windows Phone 8.0 kurudi chini ilihali kwa wenye Blackberry 10 OS wataendelea kutumia WhatsApp kwa muda wa wiki mbili na baada ya hapo app hiyo haitafanya kazi kabisa.
Ingawa kwenye Blackberry 10 OS itafanya katika kipndi cha wiki mbili zijazo lakini kuna vitu vichache vitabadilika: iwapo mtumiaji ataamua kuondoa WhatsApp na kutaka kuirudisha haitakubali au ukajaribu kusajili namba yako kwenye WhatsApp kwenye Blackberry 10 OS nyingine; haitakubali kukutumia zile tarakimu sita za kuhakiki kuwa namba uliyosajili ipo hewani.
Kwanini WhatsApp wameamua kusitisha huduma kwa baadhi ya simu janja?
Ni wazi kwamba programu endeshaji zinazotumika katika simu janja nyingi za zenye ushindani mkubwa ni Android na iOS hivyo WhatsApp wameamua kusitisha huduma ya WhatsApp kwenye simu za Windows toleo la 8.0 kushuka chini pamoja na Blackberry OS kutokana na kuwa watumiaji wengi wapo kwenye programu endeshi ya Android na iOS.
Kitu cha kufanya kuendela kupata huduma ya WhatsApp.
Kwa simu za Windows 8.0 kududi chini na Blackberry OS wanatakiwa waboreshe toleo la programu endeshi wanalotumia kwenye simu zao kwa kufanya masasisho na kuhama toleo lililofungiwa kutumia WhatsApp na kwenda toleo linalofuatia ili kuendea kutumia WhatsApp.
Kwa watumiaji wa Blackberry 10 OS baada ya kipindi cha wiki mbili kumalizika watashindwa kabisa kutumia WhatsApp kwa maana ya kwamba haitawezekana kuunganishwa na server za WhatsApp na hata WhatsApp wenyewe watazuia kabisa kutunza data za WhatsApp kwa mtu yeyote anayetumia Blackberry 10 OS.
WharsApp wanazidi kuboresha huduma zao na ili kuwa salama kabisa inashauriwa kutumia toleo la programu endeshaji kuanzia Android 4+, iOS 7+ au Windows 8.1+. Uamuzi ni wako, fanya kilicho sahihi ili kuendelea kutumia WhatsApp.
Vyanzo: Crackberry, Gadgets 360