Mtandao maarufu duniani wa Wikipedia uliojikita katika kukufahamisha mambo mbalimbali ambayo huyafahamu umetimiza miaka 14 tokea ulipoanzisha tarehe 14 mwezi wa kwanza mwaka 2001.
Katika miaka hii 14 Wikipedia imekua kwa kiasi kikubwa na imefanikiwa kubadilisha mtazamo uliokuwa umeenea sana enzi hizo ya kwamba kwa kuwa mtu yeyote anaweza andika, badilisha au kufuta kitu katika makala/taarifa basi mtandao huo ungejaa mambo ya uongo na ya kupotosha. Je ni kweli? HAPANA!
Wikipedia imefanikiwa kuonesha ya kwamba kutokana na hali ya kuwa wazi kwa mtu yeyote kufanya mabadiliko matokeo yake taarifa zinakuwa sahihi zaidi kwani mtu yeyote akigundua kosa ni rahisi zaidi kufanyiwa marekebisho kwa haraka sana kulinganisha na kwenye kitu kama kitabu kilichochapwa tayari.
Je waanzilishi ni kina nani?
Mtandao huo ulianzisha na vijana wawili wakati huo, Bwana Jimmy Wales na Larry Danger.
Kiswahili
Kuna zaidi ya makala au ‘wiki’ 28,000 yaliyoandikwa kwa lugha ya kiswahili, kwa Africa wiki za kiswahili ni za pili kwa ukubwa baada ya zile zilizoandikwa kwa lugha ya Yoruba, lugha maarufu huko Afrika magharibi.
Wiki
Neno ‘wiki’ limechukuliwa kutoka lugha ya asili ya Hawaii na lina maana ya ‘haraka/kwa haraka’, na kumbuka neno ‘pedia’ linamaana ya maharifa kwenye lugha kigiriki.
Namba 6 Duniani
Mtandao wa Wikipedia unashikilia nafasi ya sita kwenye orodha ya mitandao inayotembelewa zaidi duniani. (Kulingana na data za Alexa)
Google Inachangia sana Wikipedia
Hapa hatusemi kipesa, ila zaidi ya nusu ya matembeleo yote kwenda mtandao huo watu wanapitia kwenye kutafuta jambo kwenye mtandao wa Google.
Makala milioni 26
Kwa ujumla kwa lugha zote zinazotumika Wikipedia, kuna jumla ya makala milioni 26!
Waandishi wengi ni wanaume!
Wikipedia imetoa data zinazoonesha zaidi ya asilimia 87 ya makala yote na mabadiliko huwa yanafanywa na wanaume.
Unataka kusoma Wikipedia Yote?
Itakuchukua zaidi ya miaka 16 na miezi 9 bila kupumzika kabisa ndio utafanikiwa kumaliza kusoma makala yote yaliyopo kwenye mtandao huo.
No Comment! Be the first one.