Mwezi wa kwanza toleo la Windows 10 lilikuwa linatumika katika vifaa milioni 200 na sasa Microsoft wametoa data mpya zikionesha Windows 10 inatumika katika vifaa milioni 300. Hii ni milioni 100 zaidi katika kipindi cha miezi kadhaa tuu.
Mpango wa Microsoft wa kufanya programu endeshaji yao ya Windows 10 itumike katika vifaa bilioni 1 bado ni mbali sana lakini hadi sasa maendeleo waliyoyapata yanastahili kuitwa mafanikio tayari.
Microsoft wamesema hili huku wakisema mwisho wa mwezi wa saba mwaka huu ndio utakuwa mwisho wa uwezo wa watu kusasisha (upgrade) bure kwenda toleo la Windows 10 kwa watumiaji wa Windows 7 na 8.
Julai 29 – Tarehe ya mwisho wa upatikanaji wa bure wa toleo la Windows 10, tarehe hii itakuwa ni mwaka mmoja tokea Windows 10 kuanza kupatikana.
Je upo tayari kulipa dola $119 kwa ajili ya kupata Windows 10? Hiyo ndio bei itakayouziwa Windows 10 baada ya muda wa upatikanaji wa bure kupita.
Uamuzi wa kufanya Windows 10 ipatikane bure kwa kipindi hichi chote kinaonekana kilikuwa ni cha lazima ili kufanikisha Windows 10 kutumika. Kutumika kwa wingi kwa programu endeshaji kuna maanisha delevlopers (watengenezaji programu) wanaweza kuipa umuhimu zaidi katika utengenezaji wa programu mbalimbali.
Tushaandika mengi kuhusu toleo la Windows 10, unaweza soma uchambuzi wa programu endeshaji hii na habari zingine za Windows 10 -> Teknokona/Windows 10
Cha muhimu kufahamu ni kwamba una muda mchache tuu kabla ya Windows 10 kuacha kupatikana bure. Kuanzia sasa hadi Julai 29 utaweza kusasisha kompyuta yako inayotumia Windows 7 au 8 kwenda Windows 10 bure kabisa ata kama toleo lako la Windows ni la wizi.
Kwa pesa ya Afrika Mashariki toleo la Windows 10 baada ya muda wa kupatikana bure kuisha litapatikana kwa takribani Tsh 260,000 | Ksh 12,000.
Je ushatumia Windows 10? Unamtazamo gani juu ya programu hii ya uendeshaji?
Vyanzo: Engadget na mitandao mbalimbali
One Comment
Comments are closed.