Habari mbaya kwa watumiaji wa Windows wanaotumia diski zenye ukubwa mdogo, Windows 10 kula nafasi kubwa zaidi muda si mrefu.
Tayari watumiaji wengi wa Windows 10 wanalalamika ujio wa masasisho (updates) mbalimbali za Windows ambazo muda mwingine ndio uharibu mambo.
Microsost wamesema wanaongeza kitu kinaitwa ‘Reserved Storage’ katika toleo la Windows 10 – Build 1903. Reserved Storage, yaani Nafasi Iliyohifadhiwa itakuwa na ukubwa wa hadi GB 7 na itatumika tuu kuhifadhi matoleo ya masasisho ya Windows 10 yatakayoshushwa (download) moja kwa moja na Microsoft kutoka kwenye mtandao na kuhifadhiwa kwenye nafasi hii kabla ya mtumiaji kupewa taarifa ya kuweza kupakua/kuinstall kwenye kompyuta.
Microsoft wamesama kwa sasa teknolojia hiyo inakuja kwenye laptop mpya zitakazokuja na Windows 10 toleo la 1903 ila muda si mrefu itasambazwa kwa hata watu wanaotumia kompyuta/vipakatalishi za miaka ya nyuma. Kwa sasa kuna toleo 1809.
Suala hili hili linaleta changamoto kwa watumiaji wa aina mbili wa Windows kwa sasa;
- Wale wenye nafasi ndogo za diski, kwani GB 7 ni kiasi kikubwa sana kama diski ya kompyuta husika tayari ina vitu vingi.
- Wale wasiopenda sasisho kujidownload bila ruhusa, wengine hawapendi tuu kuhamia matoleo mapya mapema na wengine wana wasiwasi na data zao.
Vipi je, wewe ni mtumiaji wa Windows 10, una mtazamo gani na uamuzi huu wa Microsoft?
Chanzo: Forbes na tovuti mbalimbali