Ni takribani miezi miwili tokea programu endeshaji ya Windows 10 kuanza kupatikana kwa watumiaji wote, na sasa data inaonesha kuna takribani kompyuta milioni 110 zinatumia programu endeshaji hiyo.
Idadi imepungua kudogo ukilinganisha na uwezo wa kuwa kwenye kompyuta milioni 75 ndani ya mwezi wa kwanza wa kuanza kupatikana. Hii ikimaanisha katika mwezi wa pili kompyuta milioni 35 ndio zimeongezeka. Lakini bado idadi ya milioni 110 ndani ya miezi miwili ni kubwa sana na inastaili pongezi.
Kujaribu bila kupakua programu endeshaji ya Windows 10 basi tembelea – http://wndw.ms/b9HlhD
Idadi hii inafanya idadi nzima ya kompyuta zinazotumia Windows kuwa ni asilimia 6.42 ya kompyuta zote duniani. Na hii inatokana na ukweli ya kwamba toleo hili si la bure kwa wote na kwa kiasi kikubwa bado utumiaji wa Windows XP ni mkubwa na watumiaji hao hawana sifa ya kupata toleo la Windows 10.
Pia makampuni yenye sifa ya ‘Enterprises’ yanayopata huduma spesheli ya kuwekewa toleo la Windows 10 bado programu ya kuwahamisha kutoka matoleo ya zamani kuja hili jipya bado haijaanza. Watumiaji wenye sifa ya ‘enterprises’ wanatengeneza asilimia 10 ya kompyuta zote zinazotumika kwa sasa.
Je ushajaribu toleo la Windows 10? Unaweza kufuata hatua nyepesi katika mtandao wa Microsoft kuweza kupata toleo la Windows 10 – Bofya http://wndw.ms/DlmeQn . Pia unaweza kusoma chambuzi zetu mbalimbali za Windows 10 kwa kubofya – http://teknokona.com/tag/windows-10/
Vyanzo: http://www.iusbpreface.com na http://www.theinquirer.net
No Comment! Be the first one.