Hivi karibuni, mtandao wa X umetambulisha kipengele kipya kinachoitwa Makala(Article) itakayoruhusu kuchapisha maudhui marefu yenye herufi hadi laki moja. Lakini je, huu ni uvumbuzi wenye tija au la? Twende tuone!
Kipengele hiki kipya ambacho kinapatikana kwa watumiaji wa kulipia (X Premium+) na mashirika yaliyothibitishwa (verified) wanapata nafasi ya kipekee ya kuchapisha makala ndefu zenye muundo wa kuvutia, zikiweza kujumuisha picha na video.
Sio tu hivyo! Mwaka jana, X iliongeza kikomo cha herufi 25,000 kwa watumiaji wakulipia. Lakini sasa, kikomo kimeongezeka hadi 100,000 kupitia Makala(Article)! Hii inamaanisha sasa tunaweza kutiririsha mawazo yetu kwa uhuru zaidi, bila kubanwa na idadi ya herufi.
Kwa kuongezea, Makala(Article) hizi zinaweza kujumuisha picha, video, GIFs, machapisho, na viungo. Pia, unaweza kuhariri maandishi kwa kutumia vichwa vya habari, vichwa vidogo na mandishi yenye mitindo mbali mbali kama vile inavyokuwa kwenye majukwaa ya kuunda makala kama WordPress au Medium.
Hii ni habari njema kwa watumiaji wa mtaandao huo hususani wabunifu kwani itaweza kuboresha kabisha ufikishaji wa taarifa mbali mbali hivyo kuwezesha ubunifu na kuweza kuwezesha sekta ya mawasiliano kukuwa zadi!
Je wewe unamaoni ghani kuhusu uvumbuzi huu?
Tutafuatilia kwa karibu ili kuleta habari zaidi kuhusu hili na mambo mengine makubwa katika ulimwengu wa teknolojia.
Tutafuatilia kwa karibu kuhusiana taarifa hii na kukuletea habari zaidi. Endelea kuwa nasi Teknokona, kwa taarifa moto moto katika ulimwengu wa teknolojia.
Tutonane tena!
No Comment! Be the first one.