XBox ni moja kati ya kifaa cha magemu chenye watumiaji wengi na umaarufu mkubwa kabisa, kifaa hichi kinatumika na watu katika kucheza gemu.
XBox inamilikiwa na kampuni ya Microsoft na imetimiza miaka 22 tangia iingie sokoni mwaka 2001 novemba 15.
Maamuzi haya ya kampuni ya Microsoft kuingia katika hii sekta ya magemu ni moja kati ya maamuzi yenye faida kubwa sana maana kwa sasa kifaa hicho kipo katika vifaa vitatu bora vya kuchezea magemu.
Kwa muda ule mara kwa mara XBox ilikua inashindanishwa sana na Nintendo na Sony na mpambano ulikua ni mkubwa sana
Kingine kumbuka kampuni ya XBox ilikua ni hata haijuilkani kwa ukubwa huo lakini yote yalibasilika baada ya kampuni kuja na kifaa hicho cha magemu.
Kwa miaka hiyo yote kampuni imejikita zaidi katika kuboresha kifaa chake hicho na vile vile kuhakikisha wanakuja na magemu mazuri zaidi.
Ni wazi kwamba kwa sasa soko la magemu ni moja kati ya soko ambalo linatengeneza pesa nyingi sana ukilinganisha na masoko mengine.
Je wewe ni mchezaji wa magemu kupitia kifaa hiki? Niambie ni nini ambacho una kumbukumbu nacho kuhusiana na kifaa hiki cha magemu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, ninadikie hapo chini katika uwanja wa comment…….
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.