Umekaa unawaza kununua TV janja pamoja na kifaa cha michezo cha Xbox ili kupata burudani zaidi kwa wakati mmoja ila unahisi gharama inazidi kua kubwa? Basi usiwe na shaka maana Microsoft wamesema toleo jipya la Xbox kuja na apps mbalimbali kama vile Netflix na YouTube.
Kupitia matoleo la Xbox Series X na S utaweza kufurahia huduma za apps za burudani bila msaada wa kuwa na TV janja kama tulivyozoeleka hapo mwanzo. Yaani unaweza kuwa na TV ya kawaida au projekta pamoja na Xbox na ukaweza kufurahia huduma za YouTube, Netflix ama Apple Tv.
TV janja/Smart TVs ni aina ya TV zinazokuja na programu endeshaji spesheli kama vile ya Android na hivyo kuwa na uwezo wa utumiaji apps kama vile YouTube, Netflix na nyingine nyingi, huduma ambazo hazipatikani kwenye TV za kawaida.
Microsoft ndio wahusika wakuu wa utengenezaji wa vifaa cha michezo maarufu vinavyokwenda kwa jina la Xbox, Microsoft wamezidi kufanya maboresho zaidi katika vifaa vyao vya michezo vya Xbox One, Xbox series X, Xbox Series S Consoles ili kuendana na teknolojia ya wakati huu na mahitaji yake kwa watumiaji.
Vifaa vya Xbox kutoka Microsoft vinashindana kwa ukali na vile vya PlayStation kutoka Sony.
Wakati tukiendelea kusubiri uzinduzi wa Xbox SeriesX na Series S Consoles mnamo Novemba 10 mwaka huu.
Microsoft inathibitisha kuwa apps za huduma za Apple Tv, Netflix, Disney Plus, HB0 Max, Spotify, YouTube, YouTube TV, Amazon Prime Video, Hulu, NBC Peacock, Vudu, FandangoNow, Twitch, Sky Go, SASA TV, na zaidi zitapatikana kwenye toleo zote za Xbox zitazotoka mwezi huu. Pia Xbox Series X na Series S zinasapoti Dolby Vision na Dolby Atmos, ambazo ni teknolojia za kisasa za ubora wa sauti zinazofanya kazi katika huduma kama vile Netflix.
Xbox SeriesX itapatikana kwa takribani bei ya Tsh 1,157,181 ($499) wakati Xbox Series S Consoles itapatikana kwa bei ya Tsh 693,381 ($299) Novemba 10 mwaka huu. Kumbuka bei hizi huwa zinapanda vifaa hivi vikifika nchini kwa sababu za kibiashara na kodi.
Je! Nini maoni yako kuhusu maboresho hayo? Unadhani hii italeta mtazamo upi kwa watumiaji wa vifaa hivi vya michezo.
Chanzo: theverge.com
No Comment! Be the first one.