Mfululizo wa simu za Redmi Note 12 unaendelea kuleta uwezo wa kipekee (mithili ya simu za kiwango cha juu) kwa simu za kiwango cha kati, kufafanua upya upigaji picha na matumizi mengine mengi yaliyozoeleka kwa watumiaji wa simu janja.
Leo, Tarehe 20 Aprili 2023, Xiaomi imetangaza uzinduzi wa kimataifa wa mfululizo mpya wa simu za Redmi Note 12. mfululizo huu unajumuisha simu nne nzuri: Redmi Note 12 Pro+ 5G, Redmi Note 12 Pro, Redmi Note 12S, na Redmi Note 12.
Kuendeleza ubora zaidi wa mafanikio ya kushangaza ya mfululizo wa simu za Redmi Note 11, mfululizo wa simu za Redmi Note 12 unatoa uboreshaji mkubwa kwa mara nyingine kwa vipengele ambavyo vinajaliwa na mashabiki wake. Ubunifu huu ni pamoja na mfumo wa kamera, uwezo wa betri, kasi ya kuchaji na muundo mzuri kwa mtumiaji, vyote vinavyotolewa kwa thamani ya kipekee. Kwa uzinduzi wa mfululizo wa simu za Redmi Note 12 kote ulimwenguni, Xiaomi inaonyesha tena azma yake ya kufanya ufanisi wa simu za mkononi zenye kiwango cha juu kupatikana kwa watu wengi zaidi ulimwenguni.
Ufanisi wa kiwango cha juu ambavyo huhamasisha watumiaji kuishi kiuhalisia
Simu inayoongoza katika mfululizo wa simu za Redmi Note 12 ni Redmi Note 12 Pro+ 5G yenye mfumo wake hodari wa kamera tatu. Ikiwa na kamera kuu ya 200MP kama za simu za viwango vya juu yenye OIS, kamera pana na kamera ya macro, hichi ni kifaa cha juu kabisa kinachokusudia kubadilisha upya uchukuzi wa picha kwa simu za mkononi za kiwango cha kati. Redmi Note 12 Pro 5G pia huonyesha uzoefu mzuri wa picha, kwa kutoa kifaa cha IMX766 kikubwa na hodari chenye OIS, kamera pana na kamera ya macro kwa ajili ya picha nzuri hata katika mazingira ya chini ya mwanga. Ikiwa programu yenye nguvu ya algorithms za AI, kasi ya hali ya juu ya usimamizi wa mchakato wa picha na huduma zingine za kazi za utumiaji muhimu, hii inakamilisha ufanisi wa utumiaji wa kamera.
Redmi Note 12 Pro+ 5G itafurahisha watumiaji wake kwa skrini zake za 120Hz Flow AMOLED ambazo ni angavu na zenye rangi nzuri, zikiwa na msaada wa Dolby Vision® na Dolby Atmos®. Kwa vifaa vyake vya P-OLED vinavyowezesha uwepo wa mipaka finyu, Redmi Note 12 Pro+ 5G inatoa uwezo bora wa kuona na kufurahia simu.
Redmi Note 12 Pro+ 5G inakuja na kasi ya kuchaji ya ngazi ya juu, ikiwa na 120W HyperCharge na betri inayodumu muda mrefu ya 5,000mAh, inayoweza kukidhi mahitaji ya matumizi ya kila siku hata kwa matumizi ya maudhui mengi. Utendaji wa 5G bora na imara unahakikishwa na chipset ya MediaTek Dimensity 1080 yenye uwezo mkubwa.
Redmi Note 12 Pro+ 5G inaanza kwa bei ya TZS 1,000,000, na itapatikana kutoka kwa kampuni za mtandao wa simu wa Tigo na Vodacom pamoja na Masoko ya Umma ya IR kutoka Mei 2023.
Pata uzoefu wa utendaji ulio wa kushangaza kila wakati
Kila mwanafamilia wa mfululizo huu anazidi matarajio yaliyopo katika kiwango cha bei yake. Redmi Note 12 inatoa utendaji wa kushangaza na ubora wa burudani. Kwa kujivunia skrini zenye ubora wa picha zenye uwezo wa 120Hz AMOLED, watumiaji wanapata ubora wa picha maridadi na rangi sahihi. Iliyopewa nguvu na Snapdragon® 685 Mobile Platform, operesheni ni laini na isiyo na vikwazo, kuruhusu utendaji kazi mbali mbali kwa wakati mmoja kuwa rahisi na kwa ufanisi mkubwa.
Redmi Note 12 ina uwezo wa kuchaji kwa haraka wa 33W na betri yenye uwezo wa 5,000mAh (typ), maana yake watumiaji wanaweza kutumia programu nyingi na kupiga picha nyingi bila wasiwasi wa betri kuisha. Kwa kuongezea zaidi ina kamera ya AI tatu thabiti, uwezo wa kupiga picha za usiku pamoja na mfululizo wa vipengele na filta za kufurahisha, Redmi Note 12 ina kamera yenye nguvu ambayo hapo awali ilikuwa inapatikana kwa simu za kifahari, sasa inapatikana kwa watumiaji zaidi kwa bei nafuu.
Redmi Note 12 inaanza kwa bei ya 420,000 TZS, itapatikana kwenye kampuni za mitandao ya simu ya Tigo na Vodacom pamoja na Masoko ya IR ya Umma kuanzia katikati ya Aprili.
Kamera za kiwango cha juu za 108MP na mitindo ya filamu kwa ajili ya kupiga picha nzuri
Redmi Note 12 Pro na Redmi Note 12S zote zina kamera za kiwango cha juu kwaajili kupiga picha kumbukumbu zenye mvuto kwa undani zaidi. Redmi Note 12 Pro ina kipenyo kikubwa cha sensori ya Samsung 1/1.52-inch, pamoja na pixel binning 9-ndani ya-1 pamoja na dual native ISO na kamera ya kina ya 2MP ili kuunda kwa asili taathira ya bokeh kwa ajili picha za portraiti.
Simu zote mbili zinatoa kiwango kipya cha ubunifu kwa kutumia filta za kamera za filamu na kipengele cha ProCut. Kamera zinatoa picha safi katika mazingira yote ya mwanga, huku simu zote mbili zikiwa na kamera ya mbele ya 16MP kwa ajili ya picha safi na za asili za ‘selfie’.
Redmi Note 12 Pro ina kioo cha DotDisplay cha FHD+ cha 6.67″ na AMOLED DotDisplay cha kufikia 120Hz kwa ajili ya kubadili picha kwa wepesi bila kuchelewa. Pia inatumia teknolojia ya Dolby Vision® na Dolby Atmos® kwa ajili ya uwezo wa daraja la kwanza kwa picha na sauti.
Redmi Note 12S inaleta burudani kamili na sauti halisi ya stereo kwa ajili ya michezo ya video au kutazama video. Ikiwa na rangi za kupendeza na maudhui safi hata wakati wa mwangaza mkali, shukrani kwa skrini yake kubwa ya DotDisplay ya FHD+ ya 6.43″ yenye mwangaza wa juu hadi 1,000 nits. Kifaa hiki pia kina kipengele cha kubadili picha cha kufikia hadi 90Hz na kipengele cha kugusa hadi mara 180Hz kwa ajili ya kubadili picha kwa wepesi bila kuchelewa.
Redmi Note 12 Pro ni smartphone yenye uwezo mkubwa wa Snapdragon® 732G pamoja na teknolojia ya 67W turbocharging inayowezesha betri yenye uwezo wa 5,000mAh kudumu kwa muda mrefu wakati wa kutumia mitandao ya kijamii, kupiga picha, na kurekodi video. Hivyo, watumiaji wanaweza kufanya chochote wanachotaka mahali popote bila kuogopa kwamba betri itaisha.
Redmi Note 12S ina betri yenye uwezo mkubwa wa 5,000mAh pamoja na teknolojia ya kuchaji ya haraka ya 33W ambayo ina toa uwezo wa utendaji wa betri ulio na ufanisi na wa muda mrefu. Ikiwa Inaendeshwa na processor ya Octa-core MediaTek Helio G96 pamoja na RAM ya hadi 8GB, Redmi Note 12S inatoa utendaji bora na laini kwa watumiaji. Iwe ni kupiga picha za kuvutia sana, kurekodi video, kutazama sinema, au kupitia mitandao ya kijamii, Redmi Note 12S inatoa utendaji thabiti na wa kuaminika kwa burudani yako ya kila siku.
Redmi Note 12S inaanza kutoka Tsh 620,000, na Redmi Note 12 Pro inaanza kutoka Tsh 700,000. Zote zitapatikana kupitia kampuni za mtandao wa simu Tigo na Vodacom pamoja na Masoko ya Umma ya IR kutoka Mei 2023.
Kwa habari zingine kuhusu kampuni ya Xiaomi, tembelea Teknolojia/Xiaomi
No Comment! Be the first one.