Kampuni ya simu, Xiaomi imebainisha kuwa kwa sasa biashara yake imepanuka zaidi katika sehemu tofauti duniani mbali na Uchina.
Hayo yalibainishwa na mfanyabiashara, bilionea na mmiliki wa kampuni hiyo ya Xiaomi, Bw. Lei Jun wakati wa jukwaa la biashara na uwekezaji lililofanyika Shanghai ambapo masoko ya Xiaomi nje ya Uchina yamefikia takribani 82 na matano kati yao yakiwa ya kiwango cha juu kati ya masoko 25 makubwa duniani.
Soko la simu za Xiaomi zimeendelea kukua hususani robo ya pili ya mwaka 2018 kwa kukua kwa asilimia 150 ingawa wengi wakisema kampuni hiyo bado ni ndogo.