Yahoo imekuwa ikiwa nyuma kidogo katika dunia ya teknolojia – inavyoonekana – na kutokana na hili kampuni limeamua kujiweka sokoni ili kutafuta mteja wa kulinunua.
Katika swala zima la wateja, makampuni mengi yameonyesha nia zao na mengine yakionyesha nia zaidi kuliko wenzao. Kama moja kati ya kampuni itafikia vigezo na masharti vya Yahoo basi italinyakua kampuni hilo.
Wanaonekana kutaka kuinunua;
Google imeripotowa kuwa mmoja kati ya wale wenye nia ya kulinunua kampuni hilo lakini vyanzo vingine vinasema kuwa, biashara hii ina mwanya kidogo wa kutokea.
– Verizon
Ukiachana na makampuni mengine yote ambayo yameweka nia kampuni la Verizon ndio linaonekana kuwa na shauku kubwa katika kulinunua kampuni la Yahoo.
Wawakilishi wa Yahoo inasemekana waliongea na kampuni ya Facebook ikiwa ni katika mkakati wa kuwaambia waingie katika kinyang’anyiro hicho. Vyanzo vingine vinasema kuwa kampuni ya Facebook sio lazima ijiingize katika kununua kampuni hiyo kwani mpaka sasa ipo katika mstari wa mbele.
Twitter kwa upande mwingine imeonyesha kuwa inalichukulia jambo hili kwa umakini sana kwani hata wameripotiwa wakiwa waonaongea na watuwa nje juu ya jambo hili. Pia wakuu wa Twitter wamekuwa wakiongelea juu ya kutumia Yahoo ili kuwezesha shughuli za matangazo za Twitter
– Time
Hata kampuni ya Time linafikiria kuweka pesa yake ili kulinunua Yahoo. Licha ya time kuna makampuni kama vile Brian & Company na TPG ambayo pia inasemekana yana mpango huo. Makampuni haya yanaweza yakalinunua kampuni hilo moja kwa moja au kwa kupitia mgongo wa kampuni lingine.
– SoftBank
Licha ya kuwa Soft Bank inamiliki hisa za kampuni ya Yahoo tawi la Japan bado SoftBank amejitutumua na kuonyesha nia yake ya kutaka kulinunua kampuni hilo.
Tawi la Yahoo Japan limekuwa likijiendesha huru kwa miaka mingi
Kama utakuwa unakumbuka vizuri mwaka 2008 kampuni ya Microsoft ilitoa ofa ya kununua kampuni ya Yahoo kwa dola bilioni 45 za kimarekani lakini Yahoo wakakataa ofa yao. Kwa sasa Microsoft wamejiweka pembeni kabisa na mchakato mzima
Hapo mwanzo ununuzi wa Yahoo ulitakiwa kumalizika Aprili 11 mwaka huu, lakini baada ya kampuni kuona inabidi makampuni mengine yafikirie kwa kina kabla hayajaamua maaumuzi yeyote ikaamua kusogeza muda mbele
Muda umesogezwa mpaka tarehe 18 Aprili mwaka huu ambapo ndani ya muda huo (11 – 18) tunaweza tukawa tumeshapata kumjua mnunuzi wa kampuni hilo.