Yahoo! imesogeza tarehe ya mwisho ya kupokea zabuni kutoka kwa wazabuni ambao wana malengo yua kuinunua kampuni hii, badala ya tarehe 11 mwezi huu wazabuni watakuwa na mpaka tarehe 18 kwa mujibu wa vyanzo vilivyoripoti taarifa hii.
Yahoo! ambayo ni kampuni kubwa ya teknolojia ya kimarekani ambayo wengi wanaijua kwa kupitia huduma yake ya barua pepe ambayo ni moja ya mambo yaliyoifanya kampuni hii ifikie mafanikio makubwa zaidi mwaka 2008.
Kutoka mwaka 2008 kampuni hii imekuwa ikifanya vibaya kibiashara na imekuwa ikishuka katika chati, wengi wanainyoshea kidole ushindani ambao uliletwa na kampuni ya Google kuwa ndiyo hasa sababu ya kushindwa kwa Yahoo!. Ingawa yamekuwapo mafanikio ya hapa na pale lakini kimsingi biashara ya kampuni hii ambayo inafanya biashara kama ile inayofanywa na Google imekuwa mashakani kwa kipindi kirefu.
Mwanzoni mwaka huu bodi ya wakurugenzi wa kampuni hii waliamua kuiweka mnadani kampuni hii na kuwataka wateja ambao wana matumaini na kampuni hii kuwasilisha zabuni zao tayari kwaajiri ya kumtafuta mzabuni anayeweza kufikia masharti.
Hatua ya kuiweka kampuni hii katika mnada ilikuwa na kila ishara kwamba bodi ya wakurugenzi hao wamekata tamaa na jitihada za mwanamama Marissa Mayer ambaye amekuwa katika jitihada za kuirudisha kampuni hiyo katika chati lakini jitihada zake zimekuwa tasa.

Hii sasa itakuwa ni wiki moja ndefu kwa wadau wakubwa wa Yahoo hasa ambao wamewekeza hisa zao katika kampuni hii kwani baada ya tarehe 18 tutajua ni kampuni gani zitakuwa zimeingia katika mchakato wa kuinunua.
Mpaka sasa tetesi zinaonesha makampuni kadhaa yanaonesha kutaka kuichukua yahoo makampuni hayo ni kama vile Verizon na AT&T ambayo ni makampuni makubwa ya simu nchini marekani.
Makala hii imeandikwa kwa msaada wa vyanzo mbali mbali katika mtandao hasa CNBC
One Comment
Comments are closed.