YouTube ni moja kati ya mitandao ya kijamii yenye umaarufu mkubwa na inajihusisha zaidi na maswala ya video
Ni wazi kwamba mara nyingi unakua katika mtandao wa YouTube (umezubaa tuu) na hujui kitu cha kuangalia –hii inanikutaga sana mimi!
Kwa hali hii YouTube ina mpango wa kuja na kipengele ambacho kitamsaidia mtu kuweza kubofya sehemu na kuweza kuletewa video ya kuangalia.
Kipengele hiki kwa sasa kipo katika hatua ya majaribio na kinapatikana kwa baadhi ya vifaa vya simu ambavyo vina App ya YouTube.
Kingine ni kwamba kwa sasa kipengele hiki kinawapeleka watazamaji kwenda kuangalia baadhi ya video katika YouTube Shorts (video fupi fupi) tuu.
Pengine hili hapo baadae litaweza kubadilika na watumiaji watakua na uwezo wa kuangalia mpaka zile video ambazo ni ndefu.
Kizuri kuhusiana na kipengele hiki ni kwamba kitazidi kuwavuta watumiaji wa mtandao huo kuweza kubaki katika mtandao huo.
Kinachoonekana hapa ni kwamba mtandao wa YouTube utakua na uwezo wa kusoma mtumiaji haswa kwa zile video ambazo anapenda kuziangalia na kisha kama ataingia kupitia kipengele hicho basi anaweza onyeshwa video zinazofanana na zile anazopenda.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hii umeipokeaje?.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.