YouTube ni mtandao wa kijamii wenye jina kubwa sana na unasifika kwa mambo mengi ikiwemo ushambazaji wa picha n.k lakini kubwa kabisa ni usambazaji wa video kupitia mtandao huo na wengi mnakifahamu kipengele cha YouTube Stories.
Licha ya YouTube Kuwa na vipengele vingi imeonekana dhahiri kwamba wanapunguza baadhi ya vipengele katika mtandao huo na kwa sasa ni zamu ya YouTube Stories.
Hii imetangazwa na wao wenyewe kwamba kipengele cha Stories wanaachana nacho kabisa, sababu kwanini wanachukua hatua hiyo ambayo pengine itawaumiza wengi wanayo.
Kipengele cha Stories kinaondolewa kwa makusudi kabisa ila kuvipa vipaumbele vingine viwili ambavyo ni:
- YouTube Shorts
- Community Posts
Kwa mara ya kwanza kabisa stories zilianza kupatikana ndani ya mtandao huo mwaka 2018 na hazina utofauti mkubwa kama zile zinazopatikana ndani ya mtandao wa Instagram, WhatsApp au hata Snapchat (ambae ndio wa kwanza kuja na stories)
Kumbuka Stories huwa zinapotea lakini YouTube Shorts (video fupi fupi) huwa hazipotei ndani ya mtandao huo na hata Community post ni vivyo hivyo.
Mpaka kufikia tarehe 6 mwezi juni mwaka 2023 kipengele cha kutengeneza stories mpya katika mtandao wa YouTube hakitakuwepo kabisa.
YouTube wenyewe wameweka wazi kwamba Stories ambazo zitakua tayari zimepanda katika mtandao huo kabla ya maamuzi hayo hayajachukuliwa basi zinaweza zikaonyeshwa mpaka siku saba tuu –tokea zipandishwe.
Community Posts wengi huwa wanazitumia kama sehemu ya kutoa taarifa ndogo ndogo tuu –wasanii wengi huwa wanatumia kipengele hiki.
YouTube pia wameweka wazi kwamba kutakua na vitu vya kuongeza katika Shorts na Community Posts kadri ya muda uunavyozidi kwenda.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhi ni sahihi kabisa kwa mtandao huo kutoa kipengele chake ambacho kimejipatia umaarufu sana? Niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.