YouTube Shorts ni kipengele ambacho hakina muda mrefu katika mtandao wa YouTube na dhumuni lake ni kuonyesha video fupi fupi ambazo zimepewa jina hilo la shorts.
Ni wazi kuwa kuna waandaji wa maudhui wengi sana na kama unavyojua katika video za kawaida wenye maudhui yao huwa wanalipwa pindi kama kuna matangazo yataonekana juu ya maudhui yao katika mtandao wa YouTube kwa muda mrefu wale wa Youtube Shorts walikua wamesahaulika.
Kwa taarifa zilizopo ni kwamba kuanzia februari 1 mwaka 2023 kampuni itaanza kuwalipa waandaaji wa maudhui katika mtandoa huo kupitia katia kipengele cha Youtube Shorts.
Ili hili kuwezekana waandaji wa maudhui wote itabidii kukubaliana na sera kwa kuingia katika makubaliano mapya na YouTube ambayo yatawapelekea kuruhusu au kukataza kupata pesa kupitia katika maudhui katika video vya Shorts.
Kwa haraka haraka ni kwamba Youtube inachofanya ni kugawana hela wanazopata kupitia matangazo yanayoruka kupitia katika mtandao wake haswa katika video za Shorts (kuanzia tarehe moja)
Pesa hizo za matangazo watakua wakigawana na wazalishaji wa maudhui wa video hizo za shorts. Huduma ya Shorts ilianzishwa mwaka 2021 na tangia kuanza kwake kulikua na njia zingine kabisa za kuwawezesha waandaji wa maudhi wa Shorts.
Njia walizokua wakitumia ni kama vile kuunganisha na biashara za mtandaoni (mfano maduka n.k), na njia nyingine nyingine ambazo ziikua ni tofauti kabisa na hazina malipo makubwa ukilinganisha na wazalishaji wa maudhui wengine kama katika mtandao wa TikTok.
Naam hili ni jambo zuri sana na litakua na msaada wa juu kwa waandaaji wa maudhui, kumbuka kuna wengine huwa wanategemea kabisa mitandao hii ya kijamii katika kuhakikisha kuwa wanaendesha maisha yao.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani malipo yatakua ni makubwa tuu kama yake yanayopatikana katika video za kawaida katika mtandao wa YouTube.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.