YouTube ni wazi kabisa kwamba haipatani kabisa na vizuizi vya matangazo na kwa sasa bado wanaendelea na mapambano hayo.
Kumbuka kwamba kwa matangazo ni moja wapo ya njia ambayo inasababisha hata waandaji wa maudhui katika mtandao huo wa YouTube kuwa wanalipwa.
Taarifa iliyotoka hivi karibuni ilikua inasema kwamba YouTube inafunga taratibu kwenye vivinjari ambavyo sio Chrome.
Lakini baada ya muda kidogo mtandao huo ulikuja na taarifa ikikanusha na kusema kwamba inachelewa kufunguka kwa vivinjari vyote ambavyo vina teknolojia ya kuzuia matangazo (Ad Blockers).
Youtube kwa ukubwa kabisa wanategemea mapato yanayotakana na matangazo hivyo kama huitaji matangazo unashauriwa kuhamia katika YouTube Premium – ambayo ni huduma ya kulipia na haina matangazo.
Hapo mwanzo ilidhaniwa kwamba google wanafanya hivyo makusudi ili kufanya watu wengi wawe wanatumia kivinjari chake cha chrome –jambo ambalo wamekanusha.
Mtangazo yana nafasi yake na hayapingiki kabisa hivyo ni bora wadau kuvumilia tuu au kulipia huduma hiyo ambayo haina matangazo.
Soma zaidi kuhusiana na YouTube na Ad Blockers >> HAPA <<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je unahisi mtandao huo umejitetea na ulifanya kusudi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.