YouTube ni mtandao wa kijamii namba moja katika maswala ya video, mtandao huu ni maarufu sana na mara kwa mara kuna matangazo yanapita katika video hizo.
Ni wazi matangazo yanakera na kuna muda yanakera sana ila kwa mitandao ya kijamii hii ndio njia kuu ya kuhakikisha kuwa makampuni hayo (mfano YouTube) yanajipatika kipato kizuri.
Kuna baadhi ya watu huwa wanatumia njia mbadala za kuhakikisha kuwa wanazuia matangazo hayo kutoonekana wakiwa wanatazama video katika mtandao huo.
Njia hizo ambazo zinatumika ni njia mbadala na sio njia rasmi kutoka katika kampuni ya YouTube –mfano wa njia rasmi ni kama vile kujiunga na huduma ya YouTube Premium.
Kwa kampuni hili ni jambo zuri sababu inawafanya watu wengi ambao hawapendi kuona matangazo basi kuhamia katika huduma ya YouTube Premium na sio kutumia huduma zingine za kuzuia matangazo ambazo haziko rasmi.
Hapa swala ni moja tuu kama hutaki matangazo hakuna shida inakubidi kulipia tuu na kuanza kutumia huduma ya YouTube Premium ambao ina minofu ya kutosha ukilinganisha na huduma yake ya kawaida.
Wao YouTube wanajitetea kwamba matangazo katika huduma yao ni jambo la msingi sana na ndio inafanya mtandao huo upatikane duniani kote bureeeeeeeee kabisa.
Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je wewe matangazo huwa yanakukera kwa kiasi gani? Na je uko tayari kulipia huduma ya mtandao huu ili kuepukana tuu na matangazo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.