Moja ya kitu ambacho kinawashangaza wengi ni kwamba mtandao huo wa YouTube umefanya maamuzi hayo ya kuongeza bei ya kifurushi bila kutoa taarifa kwa watumiaji wake.
YouTube wameongeza $2 kwa gharama ile ya mwanzo hali ambayo imepelekea bei kupanda mpaka kufikia dola 14 za kimarekani kwa mwezi.
Gharama hii itaanza kuwaumiza wateja wapya au wanajiunga na kifurushi kwa mara nyingine huku wale wa ambao wanaendelea na kifurushi kilicholipwa hawataguswa mpaka wamalize kifurushi hicho.
Kumbuka huduma ya YT premium inafanya kazi kama YouTube ya kawaida tuu ila inakua ina vipengele ambavyo imependelewa kama vile kutoonuesha matangazo n.k
Soma Zaidi Kuhusu YouTube Premium >>HAPA<<
Kingine ni kwamba kampuni haikuishia hapo bali imeongeza mpaka gharama ya kifurushi ch amwezi cha YouTube Music kwa dola moja ya kimarekani.
Vifurushi vyote vya huduma tajwa vimeongezwa bila ya kampuni kuweka wazi sababu za kufanya hivyo bali vimeongezwa bila ya kampuni kusema chochote.
Taarif aya badiliko la bei limebadilishwa katika tangazo la kujiunga na huduma ya YouTube Premium moja kwa moja.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani ni sawa kwa kampuni kuongeza gharama ya kifurishi bila kuwataarifu watumiaji? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.