Youtube kupitia mkurugenzi wake mkuu Susan Wojcicki wametangaza kwamba wamebuni upya kitumizi chake kwaajili ya simu na tableti ili kurahisisha matumizi yake, sasa watumiaji wa kitumizi hiki wataweza kufanya mambo mengi zaidi kwa urahisi kushinda ilivyokuwa hapo mwanzo. Mabadiliko haya utakuwa umeyaona iwapo unatumia Android na ume update kitumizi hicho kuanzia usiku wa kuamkia leo.
Kwa sasa kitumizi hiki kitakua na kurasa maalumu tatu, Nyumbani (home) hapa pameundwa kukupa urahisi wa kuangalia video na kupata video za kuangalia kutoka katika mapendekezo ambayo yanatokana na video ambazo huwa unapendelea kuangalia.
Kurasa ya pili ni Subscription hapa utaweza kuona video zote zilizotolewa na chaneli ulizojiunga nazo, kwa maana hiyo sasa hatutahitaji kwenda katika chanel husika kuona video walizozitoa ilimladi ulisha jiunga na chaneli basi utaona video zao katika ukurasa huu.
Akaunti; hii ni kurasa ya tatu katika kitumizi hichi kilichobuniwa upya, hapa ni ukurasa wako wewe video zako zote ulizo pakia mtandaoni. katika kurasa hii utaweza kuhariri video kwa ajili ya kuzipakia, sasa uwezo wa kuhariri video umeongezwa hivyo kwa kutumia kamera yako ya simu unaweza kutengeneza video bora kwa msaada wa Youtube.
Pakua sasisho la app hii na utuambie mtazamo wako kwa mabadiliko haya, je umeyapenda? nini umekifurahia zaidi?
No Comment! Be the first one.