Youtube imeamua kutengeneza tovuti na application mahususi kwaajiri ya wapenda magemu kuangalia na kushiriki matangazo ya moja kwa moja. Huduma hiyo ambayo imepewa jina la YouTube Gaming itahusisha tovuti na app mpya ambavyo kwa pamoja vitawaunganisha wapenda games na tamaduni zake.
Huduma hii ambayo inatarajiwa kuachiwa mwishoni mwa kipindi cha majira joto huko marekani,itawaruhusu wachezaji na magemu kuwa na kurasa zao kama ilivyo kwa mitandao mingine hivyo kujichanganya na marafiki na pia kuzifuatilia gemu unazozipenda. Kutakuwa na takribani akaunti 25000 za gemu mbali mbali katika tovuti hii mpya.
Tovuti hii itakuwa ni mwanzo wa vita baina ya google (ambao ni wamiliki wa youtube) na mahasimu wao Amazon ambao ndio wa miliki wa Twitch. Google wanategemea saana watumiaji wa Twitch watahamia tovuti ya magemu ya youtube. Twitch ambayo inatakiribani miaka minne tangu ilipoanzishwa mnamo mwaka 2011, mwaka huu ilifikisha wastani ya wageni milioni 100 kwa mwezi.
Wakosoaji wa Google wanaona hii pia ni maneno matupu kama ilivyokuwa kabla ya kutoa hangout ambapo ilitabiliwa makubwa ikiwapo ya kuzizidi kete huduma zingine za kutuma ujumbe kama WhatsApp na Viber lakini ilipokuja haikupendwa na haikufanya yaliyotabiriwa.
<
p style=”margin: 0in; font-family: Calibri; font-size: 11pt; text-align: justify;”>Tuambie maoni yako, na endelea kutembelea mtandao wa TeknoKona!
No Comment! Be the first one.