Ndio kuna huduma ya Youtube ya kulipia ambayo ni tofauti na huduma ya kawaida ambayo wengi wameizoea.
Hapa naongelea kwa watumiaji wa huduma ya YouTube Music Na Premium na wale wateja wote ambao wanatumia huduma hizo kama sehemu za majaribio (free trial).

Kwa sasa mtandao unakua katika miongoni mwa mitandao mikubwa kabisa ya kutoa huduma ya muziki kwa mfumo wa ku’stream.
“tumekua tukiweka watu mbele katika kuhakikisha kuwa wanapata huduma nzuri, huku tukiwa tunaboresha uzoefu wao katika kutumia huduma zetu’’ – alisema Adam Smith kutoka Youtube.
Kingine ni kwamba kampuni inasema bado inafanya juu chini katika kuhakikisha kuwa mtandao wa YouTube unabaki kuwa ni sehemu pendwa kwa msikilizaji wa mziki na hata kwa msanii mwenyewe.

Hii ni hatua nzuri kwa mtandao huo maana kwa sasa kuna mitandao mingi ya aina hii na kama namba zake zinaongezeka hii inamaanisha dhahiri kuwa mtandao unafanya vizuri.
Kingine cha kujua ni kwamba huduma ya YouTube Music iko kwa kipindi cha muda mrefu sana, yaani tokea 2015 lakini usishangae kusikia kwamba iko nyuma kwa mitandao kama Apple Music, Spotify, Tidal, na mingine mingi tuu.
Je huduma hizi –YouTube Premium Na YouTube Music – zinakuchanganya?
Kwa haraka haraka ni kwamba watumiaji wa huduma ya YouTube Premium wanalipia dola za kimarekani 11.99 kwa mwezi.
Malipo hayo yanawafanya kuwa na uwezo wa kutazama video na kushusha (download) video ambazo hazina matangazo katika mtandao huo na vile vile kugusagusa katika YouTube Music.

Licha ya kufikia katika rekodi yake hii mpya ni kwamba bado iko nyuma kwa makampuni mengine mengi tuu lakini imewahakikishia watu kuwa bado inaendelea kupambana ila kuzidi kuleta ushindani na pia kuhakikisha kuwa inapata nafasi za juu zaidi
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je ushawahi kutumia huduma hizi za YouTube Premium au hata YouTube Music?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.