Instagram ni maarufu duniani kote na ina zaidi ya miaka 11 tangu iletwe kwa watumiaji lakini programu hiyo tumishi haipo kwenye iPad.
Unaweza ukashangaa kuwa kwa zaidi ya miaka 11 Instagram imekuwa ikitumika lakini programu tumishi husika “Halina” toleo mahususi la kutumika kwenye iPad. Wenye iPad na wanaotumia Instagram wataasema wanaweza kuingia kwenye akaunti zao lakini ukweli ni kwamba kwa sasa hilo linawezekana kwa njia mbili tu: Mosi, kupitia kivinjari. Pili,kwa kutumia toleo la Instagram kwenye iPhone ila hadi sasa hakuna proramu tumishi (Instagram) iliyotengenezwa kwa ajili ya wenye iPad.
Kwanini hadi sasa halijatengenezwa toleo mahususi la Instagram kutumika kwenye iPad?
Watu wengi tuu wamekuwa wakijiulizwa swali hili “Kwanini hadi lwo hii hakuna toleo la Instagram mahususi kwa ajili ya wenye iPad?”. Hivi karibuni, Bw. Marques Brownlee (anatumia YouTube mara nyingi) aliuliza swali hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kiongozi anayesimamia Instagram akajibu:
Kwa sasa Instagram haina watumiaji wengi wanaoitumia kupitia iPad kiasi chao wao kuweka kipaombele cha kutengeneza toleo mahususi kwa ajili ya iPad……..watu wengi wengi wa Instagram wanaongea mengi kupitia jumbe za maandishi kuliko kupandisha vitu na wengine wavione.
Mwonekano wa Instagram kwenye iPad kupitia kivinjari.
Haya sasa habari hii itasitisha swali linalohusu kuwepo kwa programu mahususi kwa wale ambao wanatumia bidhaa hiyo inayotengenezwa na Apple.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.