Vita za makampuni ya simu katika kujiongezea asilimia katika soko (wateja) ni moja ya vita ninavyovipenda sana. Kwa sababu kwa namna moja au niyingine zinaongeza ufanisi, ubunifu na kutushushia gharama sisi watumiaji, kwa nini usilipende jambo kama hilo?
Katika peruzi yangu katika Facebook nimekutana na taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa facebook wa Zantel siku ya leo juu ya kushusha bei zaidi kiasi ya wao kujitangaza kuwa ‘imeweka historia kwa kuzindua huduma nafuu zaidi ya mawasiliano nchini’.
Sijui kama wewe unakubaliana nao, lakini kwa jinsi walivyozitangaza naamini kwa njia moja ni kweli hizi huduma walizozitaja ni kuwa wameshusha sana, mfano huduma ya ujumbe mfupi ni sh 25 tuu!
Ni kama ifuatavyo;
• BURE – Haina haja ya usajili wa kila siku
• Piga simu mtandao WOWOTE kwa 1Tsh kwa sekunde masaa 24
• Megabaiti 50 za mtandao bure na• Kiwango cha chini kabisa cha Tsh 25 tu kwa SMS
• Piga simu bure ZANTEL kwenda ZANTEL kuanzia saa 11:00 usiku mpaka saa 6.00 ya asubuhi.
• Punguzo la asilimia 100 kwenye maduka mbalimbali nchini kwa wananchama wa Epiq
• Huduma hizi za Epiq Moto ni bure kabisa kutoka Zantel, hutakatwa kiasi chochote kwa kuzitumia.
Kitu kingine kilichonishtua zaidi yaani kiasi ya kwamba nafikiria kununua line muda wowote ni suala la call kwenda mtandao wowote ni 1Tsh/sekunde kwenda mtandao wowote, kwa kweli hadi dakika hii najiuliza hivi hiyo sio tarehe 1 April kweli? Na wasiwasi na punguzo hili, ni zaidi ya chini….lakini ngoja tuone ni mtandao gani mwingine utafuata…
Niambie wewe unaoonaje punguzo hili, je unafikiria kujiunga, kufufua line yako ya Zantel sasa?
Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa wao wa Facebook https://www.facebook.com/notes/zantel-tanzania/zantel-yaweka-historia-kwa-kuzindua-huduma-nafuu-zaidi-ya-mawasiliano-nchini/423304687709644
Nilipitia pia mtandao wao (website) www.zantel.com lakini habari hii ilikuwa haipo kule, ila nadhani itakuwa wametumia mtandao wa kijamii ili habari ziwafikie watu mapema zaidi!
No Comment! Be the first one.