Siku ni hizi kwa wengi ni vigumu kutomiliki power bank yaani betri ya ziada ya kuchajia simu au tableti yako. Umuhimu wa power bank umekua zaidi kutokana na umeme unaoweza kukatika muda wowote ila pia kwa kuwa simu janja zitu zinaweza kuisha chaji muda wowote huku tukiwa mbali na sehemu za kuchaji.
Power bank ni vifaa vinavyokusaidia kupata jinsi ya kuchaji simu au tableti yako pale unaposhindwa kuchaji kutoka vyanzo vilivyozoeleka vya umeme.
Leo naitambulisha kwako power bank kutoka kampuni ya APC.
Swali kwa nini nimefanya hivyo? Nishatumia power bank kadhaa, nyingine za bei rahisi na huku hazidumu baada ya muda mfupi, na nyingine ghari lakini ubovu upo pale pale. Kwa kifupi ni kwamba ni muhimu utumie power bank zinazohaminika na zinazotengenezwa kwa ubora, siku hizi kuna power bank nyingi sana zinazoingia kutoka makampuni ya China na kwa kiasi kikubwa nyingi zinakuwa chini ya viwango.
Power bank iliyo chini ya kiwango ina madhara makubwa kwa simu yako – itaua betri la simu yako haraka zaidi.
Kampuni ya APC ni kampuni inayotambulika kwa ubora wa vifaa mbalimbali vya elekroniki na hii ikiwa ni pamoja na betri kubwa za ziada kwa ajili ya kupeleka umeme wa uhakika kwa vifaa kama vile kompyuta n.k.
Na hivyo nilivyoona power bank yangu ya zamani niliyokuwa natumia imeanza kuwa ovyo na kushika joto sana kila napotumia basi nikaona kuchagua APC kwa kuwajaribu si vibaya. Hasa hasa kwa kuwa tayari ni kampuni yenye jina kubwa katika maeneo hayo.
Power bank zake zinazopatikana nchini zipo za aina mbili, tofauti ikiwa ni kiwango cha ujazo wa chaji kila moja inaweza kuweka pale inapokuwa imejaa. Kuna ya 5,000 mAh na ya 10,000 mAh.
Zina uwezo wa kuzuia kujichaji zaidi pale zinapojaa chaji zikiwa zimechomekwa kwenye umeme.
USB port mbili, moja ikiwa na uwezo mkubwa kwa ajili ya kuchaji tableti na nyingine ina uwezo mdogo wa umeme kwa ajili ya kuchaji simu.
Zinakuja na dhamana ya miaka miwili.
Ya 5,000 mAh
Inabebeka kiurahisi, na kutegemea na simu yako basi inaweza kuchaji hadi mara moja na nusu. Kwa tableti kama iPad na baadhi za Android basi tegemea chaji ya hadi asimilia 50. Ni kadogo kanabebeka ata kwenye mfuko wa suruali bila shida yeyote. Hichi kinakupa chaji ya kama mara mbili kwa simu janja ya kawaida.
Mimi niliipata kwa Tsh 55,000 baada ya kudai punguzo, ila kwa uhakika ukiwa na 50,000 – 70,000 kulingana na ulipo na duka husika basi unaweza pata.
Ya 10,000 mAh
Hii itakufaa kama ni mtu wa safari ndefu zaidi bila ya kuweza kuwa karibu na huduma ya umeme. Kiwango hiki ni kikubwa cha chaji na hivyo itakuwezesha kupata chaji zaidi ila kwa ukubwa wake inafanya ubebaji wake uhitaji sehemu – kama kwenye begi au pochi kwa wadada.
Bei Tsh 80,000 – 100,000.
Kuchaji – Simu mara 4, Tableti mara 1
Kutegemea na sehemu utakayonunua hakikisha unaulizia ‘warranty’, dhamana.. Ukipewa risiti unatakiwa uwe na haki ya kurudisha kama ikipata tizo ndani ya miaka miwili.
Zina uwezo wa kuzuia kujichaji zaidi pale zinapojaa chaji zikiwa zimechomekwa kwenye umeme.
Ubaya?
Zinauzwa bei ya juu sana ukilinganisha na power bank zingine zinazopatikana madukani. Kuanzia 20,000/= mtu unaweza ukapata power bank. Tofauti kuu ni usalama na uwezo wa kurudisha kama itakuwa na tatizo ndani ya kipindi cha dhamana.
Zinapatikana wapi?
Mimi nilinunua duka moja mjini. Maduka ambayo wanauza power bank hizi kwa Dar ni pamoja na Y & Z Computers – Kkoo, Ideal Computers na Masumin. Pia kwa mkoani – Gift Electronics – Morogoro na JR Electronics – Arusha. Kama umefanikiwa kuzipata katika duka jingine basi kwa kutumia eneo comment wajulishe na wengine.
Je wewe unatumia powerbank? Tuambie inaitwaje na uliinunua pande zipi? Uwezo wake wa kazi upo vipi? KUMBUKA NI MUHIMU SANA KUTUMIA POWERBANK YENYE UBORA KUEPUSHA UHARIBIFU WA BETRI YA SIMU AU TABLETI YAKO.
2 Comments