Zoom imetangaza kupitia mtandao wake kwamba imenunua kampuni ya kijerumani inayojulikana kama Karlsruhe Information Technology Solutions au kwa namna nyingine Kites GmbH.
Kampuni hii inajihusisha sana katika maswala ya tafsiri za papo kwa papo na pia Zoom inasema kuwa itaihusisha huduma hiyo kwenda sambamba na huduma yake ya kurahishisha mawasiliano baina ya watu na watu.
Kwa namna nyingine ni kwamba mtandao utakua na uwezo wa kutafsiri lugha za watu amabo wanaongea lugha tofauti na hasa hasa katika kipengele chake cha maongezi ya video ya watu wengi (video conferencing).
Kites ilianzishwa rasmi ikiwa na lengo kuu la kuwasaidia wanafunzi wa chuo darasani katika tafsiri za kiingereza na kijerumani kulingana na lugha ambazo maprofesa wao wanafundishia.
Mpaka sasa mtandao wa kijamii wa Zoom una huduma ya unukuzi (transcription) wa papo kwa papo lakini kwa sasa huduma hii ni kwa wale tuu ambao wanafanya mazungumzo kwa kutumia lugha ya kiingereza.
Katika Unukuzi bado Zoom wanakubali kwamba kuna baadhi ya madhaifu yapo na wapo tayari katika kufanya mipango ili kuona ni namna gani ambayo wanaweza boresha huduma hiyo.
Aidha Zoom wanasema kuwa mchakato unaofuata ni kuhakikisha kuwa wanafungua ofisi nchini ujerumani ili kufanya kazi na wafanyakazi wa Kaites moja kwa moja
No Comment! Be the first one.